Zechariah 1:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, kwa muda gani utaendelea kutokuwa na huruma juu ya mji wa Yerusalemu na miji ya nchi ya Yuda ambayo umeikasirikia kwa muda wa miaka sabini?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha malaika wa Mwenyezi Mungu akasema, “Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, utazuia hadi lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo yule malaika wa Bwana akajibu, akasema, Ee Bwana wa majeshi, hata lini utakataa kuurehemu Yerusalemu, na miji ya Yuda uliyoikasirikia miaka hii sabini?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, kwa muda gani utaendelea kutokuwa na huruma juu ya mji wa Yerusalemu na miji ya nchi ya Yuda ambayo umeikasirikia kwa muda wa miaka sabini?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha malaika wa BWANA akasema, “BWANA Mwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha malaika wa bwana akasema, “ bwana Mwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo yule malaika wa BWANA akajibu, akasema, Ee BWANA wa majeshi, hadi lini utakataa kuurehemu Yerusalemu, na miji ya Yuda uliyoikasirikia miaka hii sabini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, kwa muda gani utaendelea kutokuwa na huruma juu ya mji wa Yerusalemu na miji ya nchi ya Yuda ambayo umeikasirikia kwa muda wa miaka sabini?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, malaika wa Bwana alipojibu akisema: Bwana Mwenye vikosi, utaacha mpaka lini kuuhurumia Yerusalemu nayo miji ya Yuda, uliyoikasirikia hii miaka 70?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo yule malaika wa BWANA akajibu, akasema, Ee BWANA wa majeshi, hata lini utakataa kuurehemu Yerusalemu, na miji ya Yuda uliyoikasirikia miaka hii sabini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu yule malaika wa Yawe akasema: Ee Yawe wa majeshi, kwa muda gani utaendelea kutokuwa na huruma juu ya muji Yerusalema na miji ya inchi ya Yuda ambayo umeikasirikia kwa muda wa miaka makumi saba?