Zechariah 1:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, waambie watu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: Nirudieni, nami nitawarudieni nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo waambie watu: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Nirudieni mimi,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, uwaambie, Bwana wa majeshi asema hivi, Nirudieni mimi, asema Bwana wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, waambie watu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: Nirudieni, nami nitawarudieni nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyo bwana Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asema bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asema bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, uwaambie, BWANA wa majeshi asema hivi, Nirudieni mimi, asema BWANA wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, waambie watu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: Nirudieni, nami nitawarudieni nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Rudini kwangu! ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi; ndipo, nami nitakaporudi kwenu; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, uwaambie, BWANA wa majeshi asema hivi, Nirudieni mimi, asema BWANA wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, uwaambie watu kwamba: Yawe wa majeshi anasema hivi: Munirudilie nami nitawarudilia ninyi. –Ni Yawe wa majeshi anayesema.