Zechariah 1:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msiwe kama wazee wenu ambao manabii waliwaambia waachane na mienendo yao miovu na matendo yao mabaya, lakini wao hawakunisikiliza wala hawakunitii mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msiwe ninyi kama baba zenu, ambao manabii wa zamani waliwalilia, wakisema, Bwana wa majeshi asema hivi, Rudini sasa, na kuziacha njia zenu mbovu, na matendo yenu maovu; lakini hawakusikia, wala kunisikiliza, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msiwe kama wazee wenu ambao manabii waliwaambia waachane na mienendo yao miovu na matendo yao mabaya, lakini wao hawakunisikiliza wala hawakunitii mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyo bwana Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msiwe ninyi kama baba zenu, ambao manabii wa zamani waliwalilia, wakisema, BWANA wa majeshi asema hivi, Rudini sasa, na kuziacha njia zenu mbovu, na matendo yenu maovu; lakini hawakusikia, wala kunitii, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msiwe kama wazee wenu ambao manabii waliwaambia waachane na mienendo yao miovu na matendo yao mabaya, lakini wao hawakunisikiliza wala hawakunitii mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msiwe kama baba zenu walioambiwa na wafumbuaji wa kwanza kwamba: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Rudini na kuziacha njia zenu mbaya na kazi zenu mbaya! Lakini hawakusikia, wala hawakunitegea masikio; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msiwe ninyi kama baba zenu, ambao manabii wa zamani waliwalilia, wakisema, BWANA wa majeshi asema hivi, Rudini sasa, na kuziacha njia zenu mbovu, na matendo yenu maovu; lakini hawakusikia, wala kunisikiliza, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikuwe kama babu zenu. Manabii waliwaambia: Yawe anasema hivi: muachane na mienendo yenu miovu na matendo yenu mabaya. Lakini wao hawakunisikiliza wala hawakunitii. –Ni ujumbe wa Yawe.–