Zechariah 1:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa usiku, nilimwona malaika amepanda farasi mwekundu. Malaika huyo alikuwa amesimama bondeni, katikati ya miti ya mihadasi. Nyuma yake kulikuwa na farasi wengine wekundu, wa kijivujivu na weupe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa usiku nilipata maono, na tazama, mbele yangu palikuwa na mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia, na weupe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa usiku, nilimwona malaika amepanda farasi mwekundu. Malaika huyo alikuwa amesimama bondeni, katikati ya miti ya mihadasi. Nyuma yake kulikuwa na farasi wengine wekundu, wa kijivujivu na weupe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Niliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya miti ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wa usiku, nilimwona malaika amepanda farasi mwekundu. Malaika huyo alikuwa amesimama bondeni, katikati ya miti ya mihadasi. Nyuma yake kulikuwa na farasi wengine wekundu, wa kijivujivu na weupe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usiku huu nimeona mambo: nimeona mtu aliyepanda farasi mwekundu; naye alikuwa amesimama katikati ya miti ya vihagilo iliyoko huko chini bondeni, nyuma yake walikuwa farasi wekundu na wa kijivujivu na weupe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa usiku, nilimwona malaika akipanda juu ya farasi mwekundu. Malaika yule alikuwa akisimama katika bonde, katikati ya miti ya mihadasi. Nyuma yake kulikuwa farasi wengine wekundu, wa kijivujivu na weupe.