Zechariah 10:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika. Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua; ndiye awapaye watu mvua za rasharasha, na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwombeni Mwenyezi Mungu mvua wakati wa vuli; ndiye Mwenyezi Mungu atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika. Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua; ndiye awapaye watu mvua za rasharasha, na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwombeni BWANA mvua wakati wa vuli; ndiye BWANA atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwombeni bwana mvua wakati wa vuli; ndiye bwana atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA aletaye mawingu ya mvua, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi shambani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika. Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua; ndiye awapaye watu mvua za rasharasha, na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwombeni Bwana mvua siku za vuli! Bwana ndiye afanye mawingu yenye umeme; naye ndiye anayewapa matone ya mvua, majani yote ya shambani yaipate.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muombe Yawe awape mvua za masika. Yawe ndiye anayeleta mawingu ya mvua; ndiye anayewapa watu mvua za manyunyu, na kustawisha mimea katika shamba kwa ajili ya wote.