Zechariah 10:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watapitia katika bahari ya mateso, nami nitayapiga mawimbi yake, na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitavunjwa na nguvu za Misri zitatoweka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watapita katika bahari ya mateso; bahari iliyochafuka itatulizwa na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitashushwa, nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watapitia katika bahari ya mateso, nami nitayapiga mawimbi yake, na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitavunjwa na nguvu za Misri zitatoweka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watapita katika bahari ya mateso; bahari iliyochafuka itatulizwa na vilindi vyote vya Mto Nile vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitashushwa, nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watapita katika bahari ya mateso; bahari iliyochafuka itatulizwa na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitashushwa, nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watapitia katika bahari ya mateso, nami nitayapiga mawimbi yake, na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitavunjwa na nguvu za Misri zitatoweka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakapopita baharini penye masongano, atayapiga mawimbi pale baharini; ndipo, mafuriko ya maji ya jito la Nili yatakapokupwa yote, nayo majivuno ya Asuri yatanyenyekezwa, nayo bakora ya kifalme ya Misri haitakuwa na budi kutoweka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watapitia katika bahari ya mateso, nami nitayapiga mawimbi yake, na vilindi vya maji ya muto Nili vitakauka. Kiburi cha Asuria kitavunjwa na nguvu za Misri zitatoweka.