Zechariah 10:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu, na waaguzi wao wanaagua uongo; watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu, na kuwapa watu faraja tupu. Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo; wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sanamu huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo; husimulia ndoto ambazo si za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo walioteseka kwa kukosa mchungaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu, na waaguzi wao wanaagua uongo; watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu, na kuwapa watu faraja tupu. Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo; wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sanamu huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo; husimulia ndoto ambazo si za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo walioonewa kwa kukosa mchungaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sanamu huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo; husimulia ndoto ambazo si za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo walioonewa kwa kukosa mchungaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo watu wanatangatanga kama kondoo, wanateseka kwa kukosa mchungaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu, na waaguzi wao wanaagua uongo; watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu, na kuwapa watu faraja tupu. Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo; wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani vinyago husema yasiyo na maana, nao waaguaji huona yaliyo uwongo, husema ndoto zisizo za kweli, wakituliza mioyo, ni bure; kwa hiyo watu hujiendea kama kondoo, huteseka, kwani hakuna awachungaye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sanamu zao za kupigia ramuli ni uongo mutupu, na waaguzi wao wanaagua uongo; watabiri wao wanatabiri ndoto danganyifu, na kuwapa watu faraja za bure. Ndiyo maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo; wanataabika maana wamekosa muchungaji.