Zechariah 10:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji, nami nitawaadhibu hao viongozi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda. Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi; kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atalichunga kundi lake, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kama farasi mwenye kiburi akiwa vitani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu mbuzi waume; kwa maana Bwana wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji, nami nitawaadhibu hao viongozi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda. Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi; kwa kuwa BWANA Mwenye Nguvu Zote atalichunga kundi lake, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi mwenye kiburi akiwa vitani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi; kwa kuwa bwana Mwenye Nguvu Zote atalichunga kundi lake, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi mwenye kiburi akiwa vitani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi; kwa maana BWANA wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji, nami nitawaadhibu hao viongozi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda. Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wachungaji ndio, makali yangu yanaowawakia moto, nao viongozi ndio, nitakaowapatiliza; kwani Bwana Mwenye vikosi amelikagua kundi lake, ndio mlango wa Yuda, nao ndio atakaowageuza, wawe kama farasi mwenye utukufu wake katika mapigano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu mbuzi waume; kwa maana BWANA wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Nimewaka hasira juu ya hao wachungaji, nami nitawaazibu hao watawala. Mimi Yawe wa majeshi, nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda. Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.