Zechariah 10:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitani watawakanyaga maadui zao katika tope njiani. Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao; nao watawaaibisha hata wapandafarasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa wanaokanyaga barabara za matope wakati wa vita. Kwa sababu Mwenyezi Mungu yu pamoja nao, watapigana na kuwashinda wapanda farasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu Bwana yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitani watawakanyaga maadui zao katika tope njiani. Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao; nao watawaaibisha hata wapandafarasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa wanaokanyaga barabara za matope wakati wa vita. Kwa sababu BWANA yu pamoja nao, watapigana na kuwashinda wapanda farasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa wanaokanyaga barabara za matope wakati wa vita. Kwa sababu bwana yu pamoja nao, watapigana na kuwashinda wapanda farasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu BWANA yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitani watawakanyaga maadui zao katika tope njiani. Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao; nao watawaaibisha hata wapandafarasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watakuwa kama mafundi wa vita, wawakanyagao adui matopeni barabarani kwenye mapigano; watakapopigana, Bwana atakuwa nao, wawatweze waliopanda farasi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu BWANA yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa katika vita, watawakanyaga waadui zao ndani ya matope katika njia. Watapigana kwa sababu mimi Yawe nipo pamoja nao; nao watawafezehesha hata waaskari wapanda-farasi.