Zechariah 10:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu wa Yuda nitawaimarisha; nitawaokoa wazawa wa Yosefu. Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma, nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, nami nitayasikiliza maombi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nitaiimarisha nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yusufu. Nitawarejesha kwa sababu nina huruma juu yao. Watakuwa kama watu ambao sijawahi kuwakataa kwa sababu mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao, nami nitawajibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana, Mungu wao, nami nitawasikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu wa Yuda nitawaimarisha; nitawaokoa wazawa wa Yosefu. Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma, nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, nami nitayasikiliza maombi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nitaiimarisha nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yosefu. Nitawarejesha kwa sababu nina huruma juu yao. Watakuwa kama watu ambao sijawahi kuwakataa kwa sababu mimi ndimi BWANA Mungu wao, nami nitawajibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nitaiimarisha nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yusufu. Nitawarejesha kwa sababu nina huruma juu yao. Watakuwa kama watu ambao sijawahi kuwakataa kwa sababu mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wao, nami nitawajibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni BWANA, Mungu wao, nami nitawasikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu wa Yuda nitawaimarisha; nitawaokoa wazawa wa Yosefu. Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma, nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, nami nitayasikiliza maombi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawatia nguvu walio mlango wa Yuda, nao walio mlango wa Yosefu nitawaokoa, nitawarudisha kwao, kwani nitawahurumia, nao watakuwa kama watu, nisiowatupa kwani mimi Bwana ni Mungu wao, nami nitawaitikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni BWANA, Mungu wao, nami nitawasikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawaimarisha watu wa Yuda; nitawaokoa wazao wa Yosefu. Nitawarudisha kwao kwa maana ninawaonea huruma, nao watakuwa kama vile sikuwa nimewakataa. Mimi ni Yawe, Mungu wao, nami nitayasikiliza maombi yao.