Zechariah 11:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana nitaleta nchini mchungaji asiyemjali kondoo anayeangamia, au kumtafuta kondoo anayetangatanga, au kumtibu aliyejeruhiwa wala kumlisha aliye hai: Bali atakula wale kondoo wanono, hata kwato zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana ninaenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana nitaleta nchini mchungaji asiyemjali kondoo anayeangamia, au kumtafuta kondoo anayetangatanga, au kumtibu aliyejeruhiwa wala kumlisha aliye hai: bali atakula wale kondoo wanono, hata kwato zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuziraruararua kwato zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana nitaleta nchini mchungaji asiyemjali kondoo anayeangamia, au kumtafuta kondoo anayetangatanga, au kumtibu aliyejeruhiwa wala kumlisha aliye hai: Bali atakula wale kondoo wanono, hata kwato zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani utaniona, mimi nikiinua katika nchi hii mchungaji asiyewakagua waliotoweka, asiyewatafuta waliopotea, asiyewaponya waliovunjika, asiyewatunza walio wakiwa, lakini nyama za vinono atazila, nazo kwato zao ataziondoa kwa nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana nitaleta katika inchi muchungaji asiyemujali kondoo anayeangamia, au kumutafuta kondoo anayetangatanga, au kumutunza aliyeumizwa wala kumukulisha yule anayekuwa muzima: lakini atakula wale kondoo wanono, hata kwato zao.