Zechariah 11:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu nasema kwamba, sitawahurumia tena wakazi wa dunia. Nitamwacha kila mtu mikononi mwa mwenzake, na kila raia mikononi mwa mfalme wake. Nao wataiangamiza dunia, nami sitamwokoa yeyote mikononi mwao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema Bwana; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu nasema kwamba, sitawahurumia tena wakazi wa dunia. Nitamwacha kila mtu mikononi mwa mwenzake, na kila raia mikononi mwa mfalme wake. Nao wataiangamiza dunia, nami sitamwokoa yeyote mikononi mwao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema BWANA. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema bwana. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema BWANA; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitamwokoa yeyote kutoka katika mkono wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu nasema kwamba, sitawahurumia tena wakazi wa dunia. Nitamwacha kila mtu mikononi mwa mwenzake, na kila raia mikononi mwa mfalme wake. Nao wataiangamiza dunia, nami sitamwokoa yeyote mikononi mwao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Sitawahurumia tena wakaao katika nchi hii, utaniona, mimi nikiwatoa watu hawa na kuwatia kila mtu mkononi mwa mchungaji wake namo mkononi mwa mfalme wake, ndio watakaoiponda nchi hii, nami sitawaponya mikononi mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema BWANA; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sitawahurumia tena wakaaji wa dunia. Nitamwacha kila mutu katika mikono ya mwenzake, na kila mwanainchi katika mikono ya mufalme wake. Nao wataiangamiza dunia, nami sitamwokoa mutu yeyote toka katika mikono yao. –Ni ujumbe wa Yawe.