Zechariah 11:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nikawa mchungaji wa kondoo waliokuwa wanakwenda kuchinjwa, kwani niliajiriwa na wale waliofanya biashara ya kondoo. Nikachukua fimbo mbili: Moja nikaiita “Fadhili,” na nyingine nikaiita “Umoja,” nikaenda kuchunga kondoo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililodhulumiwa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nikawa mchungaji wa kondoo waliokuwa wanakwenda kuchinjwa, kwani niliajiriwa na wale waliofanya biashara ya kondoo. Nikachukua fimbo mbili: moja nikaiita “Fadhili,” na nyingine nikaiita “Umoja,” nikaenda kuchunga kondoo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa. Kisha nikajipatia fimbo mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na ya pili nikaiita, Umoja; nikalilisha kundi lile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nikawa mchungaji wa kondoo waliokuwa wanakwenda kuchinjwa, kwani niliajiriwa na wale waliofanya biashara ya kondoo. Nikachukua fimbo mbili: Moja nikaiita “Fadhili,” na nyingine nikaiita “Umoja,” nikaenda kuchunga kondoo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, nikawachunga hao kondoo walio wa kuuawa tu, nao walikuwa kondoo wanyonge kweli; nikajichukulia fimbo mbili, moja nikaiita Mapendeleo, ya pili nikaiita Mapatanisho, nikawachunga hao kondoo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa. Kisha nikajipatia fimbo mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na ya pili nikaiita, Vifungo; nikalilisha kundi lile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, nikakuwa muchungaji wa kondoo ambao wachuuzi waliwatayarisha kwenda kuchinjwa. Nikatwaa fimbo mbili: moja nikaiita “Rehema”, na ingine nikaiita “Umoja”, nikaenda kuchunga kondoo.