Zechariah 12:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Neno la Mwenyezi-Mungu kuhusu Israeli. Mwenyezi-Mungu aliyezitandaza mbingu, aliyeiweka misingi ya dunia na kumpa mwanadamu uhai asema hivi:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Neno la unabii: Hili ni neno la Mwenyezi Mungu kuhusu Israeli. Mwenyezi Mungu, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ufunuo wa neno la Bwana juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo Bwana, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Neno la Mwenyezi-Mungu kuhusu Israeli. Mwenyezi-Mungu aliyezitandaza mbingu, aliyeiweka misingi ya dunia na kumpa mwanadamu uhai asema hivi:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ni neno la BWANA kuhusu Israeli. BWANA, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ni neno la bwana kuhusu Israeli. bwana, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ufunuo wa neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Neno la Mwenyezi-Mungu kuhusu Israeli. Mwenyezi-Mungu aliyezitandaza mbingu, aliyeiweka misingi ya dunia na kumpa mwanadamu uhai asema hivi:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tamko zito la Bwana, alilowaambia Waisiraeli. Ndivyo, asemavyo Bwana aliyezitanda mbingu, aliyeuweka msingi wa nchi, aliyeiumba roho ya mtu ndani yake:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ufunuo wa neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ujumbe wa Yawe unaoelekea Israeli. Yawe aliyezitandaza mbingu, aliyeiweka misingi ya dunia na kumupa mwanadamu uzima anasema hivi: