Zechariah 12:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazawa wa Daudi na wakazi wa mji wa Yerusalemu nitawajaza roho ya huruma na maombi, nao watamtazama yeye waliyemtoboa; watamlilia kama mtu amliliavyo mtoto wake wa pekee, au kama mtu amliliavyo kwa uchungu mzaliwa wake wa kwanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wa Daudi na wakazi wa mji wa Yerusalemu nitawajaza roho ya huruma na maombi, nao watamtazama yeye waliyemtoboa; watamlilia kama mtu amliliavyo mtoto wake wa pekee, au kama mtu amliliavyo kwa uchungu mzaliwa wake wa kwanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma, nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimdunga; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazawa wa Daudi na wakazi wa mji wa Yerusalemu nitawajaza roho ya huruma na maombi, nao watamtazama yeye waliyemtoboa; watamlilia kama mtu amliliavyo mtoto wake wa pekee, au kama mtu amliliavyo kwa uchungu mzaliwa wake wa kwanza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao walio wa mlango wa Dawidi nao wenyeji wa Yerusalemu nitawamiminia Roho ya kuhurumiana na ya kuombeana; ndipo, watakaponitazama, waliyemchoma. Kisha wataniombolezea, kama watu wanavyomwombolezea mwana wa pekee, nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama mtu anavyoona uchungu kwa ajili ya mwana aliyezaliwa wa kwanza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu nitawajaza wazao wa Daudi na wakaaji wa muji Yerusalema roho ya huruma na maombi, nao watamwangalia yule waliyemutoboa kwa mukuki; watamulilia kama vile mutu anavyolia kwa kifo cha mutoto wake wa pekee, au kama vile mutu anavyomulilia kwa uchungu muzaliwa wake wa kwanza.