Zechariah 12:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nitaufanya mji wa Yerusalemu kuwa kama kikombe cha divai; na mataifa yaliyo kandokando yake yatakunywa na kuyumbayumba kama walevi. Mji wa Yerusalemu utakaposhambuliwa, hata miji yote ya Yuda itashambuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nitaenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nitaufanya mji wa Yerusalemu kuwa kama kikombe cha divai; na mataifa yaliyo kandokando yake yatakunywa na kuyumbayumba kama walevi. Mji wa Yerusalemu utakaposhambuliwa, hata miji yote ya Yuda itashambuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kulewalewa kwa mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbayumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nitaufanya mji wa Yerusalemu kuwa kama kikombe cha divai; na mataifa yaliyo kandokando yake yatakunywa na kuyumbayumba kama walevi. Mji wa Yerusalemu utakaposhambuliwa, hata miji yote ya Yuda itashambuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaniona, nikiuweka Yerusalemu kuwa chano cha kuwalevya sana wao wa makabila yote wanaokaa na kuuzunguka; hata Wayuda watapatwa na mambo, Yerusalemu utakaposongwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumba-yumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitaufanya Yerusalema kuwa kama kikombe cha divai; na mataifa yanayokuwa kandokando yake yatakunywa na kuyumbayumba kama walevi. Muji Yerusalema utakaposhambuliwa, hata miji yote ya Yuda itashambuliwa.