Zechariah 12:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo viongozi wa Yuda watakapoambiana, ‘Wakazi wa Yerusalemu wamepata nguvu yao kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ni Mungu wao.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakuu wa Yuda watasema mioyoni mwao, Wenyeji wa Yerusalemu ni nguvu zangu katika Bwana wa majeshi, Mungu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo viongozi wa Yuda watakapoambiana, ‘Wakazi wa Yerusalemu wamepata nguvu yao kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu BWANA Mwenye Nguvu Zote ni Mungu wao.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu bwana Mwenye Nguvu Zote ni Mungu wao.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wakuu wa Yuda watasema mioyoni mwao, Wenyeji wa Yerusalemu wana nguvu katika BWANA wa majeshi, Mungu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo viongozi wa Yuda watakapoambiana, ‘Wakazi wa Yerusalemu wamepata nguvu yao kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wakuu wa Yuda watakaposema mioyoni mwao: Wenyeji wa Yerusalemu ndio nguvu zetu, kwa kuwa tunaye Bwana Mwenye vikosi aliye Mungu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakuu wa Yuda watasema mioyoni mwao, Wenyeji wa Yerusalemu ni nguvu zangu katika BWANA wa majeshi, Mungu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo wakubwa wa Yuda wataambiana: “Wakaaji wa Yerusalema wamepata nguvu yao kutoka kwa Yawe wa majeshi, Mungu wao.”