Zechariah 12:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nitawalinda wakazi wa mji wa Yerusalemu; walio wanyonge zaidi miongoni mwao watakuwa na nguvu kama mfalme Daudi. Wazawa wa Daudi watashika usukani kuwaongoza watu wa Yuda kama malaika wangu mimi Mwenyezi-Mungu, naam, kama mimi Mungu mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku hiyo, Mwenyezi Mungu atawakinga wale wanaoishi Yerusalemu, ili aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa Mwenyezi Mungu akiwatangulia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nitawalinda wakazi wa mji wa Yerusalemu; walio wanyonge zaidi miongoni mwao watakuwa na nguvu kama mfalme Daudi. Wazawa wa Daudi watashika usukani kuwaongoza watu wa Yuda kama malaika wangu mimi Mwenyezi-Mungu, naam, kama mimi Mungu mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hiyo, BWANA atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa BWANA akiwatangulia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hiyo, bwana atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa bwana akiwatangulia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku hiyo BWANA atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa BWANA mbele yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nitawalinda wakazi wa mji wa Yerusalemu; walio wanyonge zaidi miongoni mwao watakuwa na nguvu kama mfalme Daudi. Wazawa wa Daudi watashika usukani kuwaongoza watu wa Yuda kama malaika wangu mimi Mwenyezi-Mungu, naam, kama mimi Mungu mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo ndipo, Bwana atakapowakingia wenyeji wa Yerusalemu, aliye mnyonge kwao siku hiyo awe kama Dawidi, nao walio wa mlango wa Dawidi wawe kama Mungu, kama malaika wa Bwana awaongozaye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku hiyo BWANA atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa BWANA mbele yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, mimi Yawe nitawalinda wakaaji wa Yerusalema. Wanaokuwa wazaifu zaidi kati yao watakuwa na nguvu kama mufalme Daudi. Wazao wa Daudi watashika usukani kwa kuwaongoza watu wa Yuda kama Mungu, au kama malaika wa Yawe.