Zechariah 13:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote akijidai kuwa nabii, baba na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Unapaswa kufa kwa kuwa unasema uongo kwa jina la Mwenyezi-Mungu’. Na haohao wazazi wake watamchoma kisu akiwa anatabiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la Mwenyezi Mungu.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la Bwana; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote akijidai kuwa nabii, baba na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Unapaswa kufa kwa kuwa unasema uongo kwa jina la Mwenyezi-Mungu’. Na haohao wazazi wake watamchoma kisu akiwa anatabiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa yupo ye yote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la BWANA.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la bwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la BWANA; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtambua atoapo unabii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote akijidai kuwa nabii, baba na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Unapaswa kufa kwa kuwa unasema uongo kwa jina la Mwenyezi-Mungu’. Na haohao wazazi wake watamchoma kisu akiwa anatabiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa, kama mtu atataka kufumbua maneno tena, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia: Hutapata kuishi, kwani unasema uwongo na kulitaja Jina la Bwana, kisha baba yake na mama yake waliomzaa watamchoma kwa ajili ya ufumbuaji wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la BWANA; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote akijidai kuwa nabii, baba na mama yake waliomuzaa watamwambia: “Unapaswa kufa maana unasema uongo kwa jina la Yawe.” Na wale wazazi wake watamuchoma kisu akiwa anatabiri.