Zechariah 13:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Amka, ee upanga! Inuka umshambulie mchungaji wangu; naam, mchungaji anayenitumikia. Mpige mchungaji na kondoo watawanyike. Nitaunyosha mkono wangu, kuwashambulia watu wadhaifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, dhidi ya mtu aliye karibu nami!” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika, nami nitageuza mkono wangu dhidi ya walio wadogo,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema Bwana wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Amka, ee upanga! Inuka umshambulie mchungaji wangu; naam, mchungaji anayenitumikia. Mpige mchungaji na kondoo watawanyike. Nitaunyosha mkono wangu, kuwashambulia watu wadhaifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Amka, Ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, dhidi ya mtu aliye karibu nami!” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. “Mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika, nami nitageuza mkono wangu dhidi ya walio wadogo,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, dhidi ya mtu aliye karibu nami!” asema bwana Mwenye Nguvu Zote. “Mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika, nami nitageuza mkono wangu dhidi ya walio wadogo,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Amka, ee upanga! Inuka umshambulie mchungaji wangu; naam, mchungaji anayenitumikia. Mpige mchungaji na kondoo watawanyike. Nitaunyosha mkono wangu, kuwashambulia watu wadhaifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe upanga, amka, umpige mchungaji wangu na mwenzangu wa bia! Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi. Mpige mchungaji, kondoo watawanyike! Nami nitaugeuza mkono wangu, uwaelekeze wadogo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi anasema hivi: Amuka, ee upanga! Simama umushambulie muchungaji wangu, muchungaji anayenitumikia. Umuue muchungaji na kondoo watawanyike. Nitaunyoosha mukono wangu kwa kuwashambulia watu wazaifu.