Zechariah 13:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Theluthi hiyo moja itakayosalia, nitaijaribu na kuitakasa, kama mtu asafishavyo fedha, naam, kama ijaribiwavyo dhahabu. Hapo wao wataniomba mimi, nami nitawajibu. Nitasema, ‘Hawa ni watu wangu’, nao watasema, ‘Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii theluthi moja nitaileta katika moto; nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia Jina langu nami nitawajibu; nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘Mwenyezi Mungu ni Mungu wetu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Theluthi hiyo moja itakayosalia, nitaijaribu na kuitakasa, kama mtu asafishavyo fedha, naam, kama ijaribiwavyo dhahabu. Hapo wao wataniomba mimi, nami nitawajibu. Nitasema, ‘Hawa ni watu wangu’, nao watasema, ‘Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii theluthi moja nitaileta katika moto; nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia Jina langu nami nitawajibu; nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘BWANA ni Mungu wetu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii theluthi moja nitaileta katika moto; nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia Jina langu nami nitawajibu; nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘ bwana ni Mungu wetu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Theluthi hiyo moja itakayosalia, nitaijaribu na kuitakasa, kama mtu asafishavyo fedha, naam, kama ijaribiwavyo dhahabu. Hapo wao wataniomba mimi, nami nitawajibu. Nitasema, ‘Hawa ni watu wangu’, nao watasema, ‘Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nalo hilo fungu la tatu nitalitia motoni, niwang'aze kwa kuwayeyusha, kama watu wanavyong'aza fedha kwa kuiyeyusha, tena nitawajaribu kabisa, kama watu wanavyojaribu dhahabu. Kisha hapo, watakapolililia Jina langu, mimi nitawaitikia na kuwaambia: Hawa ndio walio ukoo wangu; ndipo, watakapoitikia wao: Nawe Bwana ndiwe Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu hiyo moja ya tatu itakayobaki, nitaipima na kuitakasa, kama vile mutu anavyosafisha feza, kama vile wanavyopima zahabu. Halafu wao wataniomba mimi, nami nitawajibu. Nitasema: Hawa ni watu wangu, nao watasema: Yawe, ndiye Mungu wetu.