Zechariah 14:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya Mwenyezi Mungu inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, siku moja ya Bwana inakuja, ambayo mateka yatagawanyika kati yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya BWANA inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya bwana inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, siku ya BWANA inakuja, ambayo mali mliyonyang'anywa itagawanywa kati yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaona, siku ya Bwana ikija; ndipo, mateka yako yatakapogawanywa mjini mwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, siku moja ya BWANA inakuja, ambayo mateka yatagawanyika kati yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Angalia, siku ya kasirani ya Yawe inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalema, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu.