Zechariah 14:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kuhusu wale watu ambao walikuja kupigana na Yerusalemu, haya ndiyo maafa ambayo Mwenyezi-Mungu atawaletea: Miili yao itaoza wangali hai; macho yao yataoza yakiwa kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza zikiwa vinywani mwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ndiyo tauni ambayo Mwenyezi Mungu atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hii ndiyo tauni, ambayo Bwana atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu; nyama ya mwili wao itaharibika, wasimamapo juu ya miguu yao, na macho yao yataharibika ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitaharibika vinywani mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kuhusu wale watu ambao walikuja kupigana na Yerusalemu, haya ndiyo maafa ambayo Mwenyezi-Mungu atawaletea: Miili yao itaoza wangali hai; macho yao yataoza yakiwa kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza zikiwa vinywani mwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ndiyo tauni ambayo BWANA atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ndiyo tauni ambayo bwana atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hii ndiyo tauni, ambayo BWANA atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu; nyama ya mwili wao itaharibika, wakiwa wamesimama kwa miguu yao, na macho yao yataharibika ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitaharibika vinywani mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kuhusu wale watu ambao walikuja kupigana na Yerusalemu, haya ndiyo maafa ambayo Mwenyezi-Mungu atawaletea: Miili yao itaoza wangali hai; macho yao yataoza yakiwa kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza zikiwa vinywani mwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hili ndilo pigo, Bwana atakaloyapiga makabila yote yaliyopeleka vikosi vyao kupigana na Yerusalemu: ataziozesha nyama za miili yao, wakiwa wamesimama kwa miguu yao, nayo macho yao yataoza ndani ya matundu yao, nazo ndimi zao zitaoza vinywani mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hii ndiyo tauni, ambayo BWANA atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu; nyama ya mwili wao itaharibika, wasimamapo juu ya miguu yao, na macho yao yataharibika ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitaharibika vinywani mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini juu ya wale watu ambao walikuja kupigana na Yerusalema, hizi ndizo hasara ambazo Yawe atawaletea: Miili yao itaoza wangali wazima; macho yao yataoza yakiwa kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza zikiwa katika vinywa vyao.