Zechariah 14:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Iwapo Wamisri watakataa kuiadhimisha sikukuu ya vibanda, basi, Mwenyezi-Mungu atawapiga kwa ugonjwa uleule atakaowapiga nao mataifa yote yanayokataa kuiadhimisha sikukuu hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa watu wa Misri nao hawataenda kushiriki, hawatapata mvua. Mwenyezi Mungu ataleta juu yao tauni ambayo itayapiga mataifa ambayo hayataenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo Bwana atawapiga mataifa, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Iwapo Wamisri watakataa kuiadhimisha sikukuu ya vibanda, basi, Mwenyezi-Mungu atawapiga kwa ugonjwa uleule atakaowapiga nao mataifa yote yanayokataa kuiadhimisha sikukuu hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. BWANA ataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. bwana ataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo BWANA atawapiga mataifa, wasiokwea ili kuadhimisha sikukuu ya Vibanda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Iwapo Wamisri watakataa kuiadhimisha sikukuu ya vibanda, basi, Mwenyezi-Mungu atawapiga kwa ugonjwa uleule atakaowapiga nao mataifa yote yanayokataa kuiadhimisha sikukuu hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ingawa mlango wa Wamisri usipande kufika huko, basi, hata kwao mvua haitanyesha. Hilo ndilo pigo, Bwana atakalowapiga wamizimu watakaokataa kupanda huko, waile sikukuu ya Vibanda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo BWANA atawapiga mataifa, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa Wamisri watakataa kushiriki kwa sikukuu ya Vibanda, basi, Yawe atawapiga kwa ugonjwa uleule atakaowapiga nao mataifa yote yanayokataa kushiriki kwa sikukuu hiyo.