Zechariah 14:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mtakimbia kupitia bonde hilo, katikati ya milima miwili ya Mwenyezi-Mungu. Mtakimbia kama wazee wenu walivyokimbia tetemeko la ardhi wakati wa utawala wa mfalme Uzia wa Yuda. Kisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, atakuja na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, atakuja na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mtakimbia kupitia bonde hilo, katikati ya milima miwili ya Mwenyezi-Mungu. Mtakimbia kama wazee wenu walivyokimbia tetemeko la ardhi wakati wa utawala wa mfalme Uzia wa Yuda. Kisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, atakuja na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha BWANA Mungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha bwana Mwenyezi Mungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mtakimbia kupitia bonde hilo, katikati ya milima miwili ya Mwenyezi-Mungu. Mtakimbia kama wazee wenu walivyokimbia tetemeko la ardhi wakati wa utawala wa mfalme Uzia wa Yuda. Kisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, atakuja na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi mtapata kukimbilia mle bondeni kwenye milima yangu, kwani hilo bonde la milima yangu litakwenda kufika mpaka Aseli; nanyi mtakimbia, kama mlivyoukimbia ule mtetemeko wa nchi siku za Uzia, mfalme wa Yuda. Kisha Bwana Mungu wangu atakuja, nao watakatifu wote watakuwa pamoja na wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi mutakimbia kupitia bonde lile, katikati ya milima miwili ya Yawe. Mutakimbia kama vile babu zenu walivyokimbia tetemeko la inchi wakati wa utawala wa mufalme Uzia wa Yuda. Kisha Yawe, Mungu wangu, atakuja na watakatifu wote pamoja naye.