Zechariah 2:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mataifa mengi yatajiunga nami Mwenyezi-Mungu, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yenu.” Mambo hayo yatakapotukia ndipo mtakapojua kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndiye aliyenituma kwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mataifa mengi yataunganishwa na Mwenyezi Mungu siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu, nanyi mtajua kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amenituma kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mataifa mengi yatajiunga nami Mwenyezi-Mungu, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yenu.” Mambo hayo yatakapotukia ndipo mtakapojua kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndiye aliyenituma kwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mataifa mengi yataunganishwa na BWANA siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba BWANA Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mataifa mengi yataunganishwa na bwana siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mataifa mengi watajiunga na BWANA katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mataifa mengi yatajiunga nami Mwenyezi-Mungu, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yenu.” Mambo hayo yatakapotukia ndipo mtakapojua kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndiye aliyenituma kwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo itakuwa, wamizimu wengi waje kuandamana na Bwana; ndipo, wao nao watakapokuwa ukoo wangu. Nitakaa katikati yako, upate kujua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma kwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mataifa mengi watajiunga na BWANA katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haraka! Ninyi wote munaokaa katika inchi ya Babeli, mukimbilie Sayuni!