Zechariah 3:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika maono mengine, Mwenyezi-Mungu alinionesha kuhani mkuu Yoshua amesimama mbele ya malaika wa Mwenyezi-Mungu, na upande wake wa kulia amesimama Shetani kumshtaki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akanionesha Yoshua, kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Mwenyezi Mungu, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika maono mengine, Mwenyezi-Mungu alinionesha kuhani mkuu Yoshua amesimama mbele ya malaika wa Mwenyezi-Mungu, na upande wake wa kulia amesimama Shetani kumshtaki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akanionyesha Yoshua, Kuhani Mkuu akiwa amesimama mbele ya malaika wa BWANA, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshitaki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa bwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akanionesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kulia ili kushindana naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika maono mengine, Mwenyezi-Mungu alinionesha kuhani mkuu Yoshua amesimama mbele ya malaika wa Mwenyezi-Mungu, na upande wake wa kulia amesimama Shetani kumshtaki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akanionyesha mtambikaji mkuu Yosua, akisimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Satani alikuwa amesimama kuumeni kwake kumsengenya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika maono mengine, Yawe alinionyesha Kuhani Mukubwa Yoshua akisimama mbele ya malaika wa Yawe, na kwa upande wake wa kuume Shetani alisimama kwa kumushitaki.