Zechariah 3:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Ukifuata mwongozo wangu na kuyazingatia maagizo niliyokupa, basi, utaisimamia nyumba yangu na nyua zake. Nami nitakuwezesha kuingia katika utumishi wangu kama hawa wanaosimama mbele yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Ikiwa utatembea katika njia zangu na kushika maagizo yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi asema hivi, Kama ukienda katika njia zangu, na kama ukishika maagizo yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba yangu, nawe utazilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Ukifuata mwongozo wangu na kuyazingatia maagizo niliyokupa, basi, utaisimamia nyumba yangu na nyua zake. Nami nitakuwezesha kuingia katika utumishi wangu kama hawa wanaosimama mbele yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hivi ndivyo asemavyo bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi asema hivi, Ikiwa utaenda katika njia zangu, na kushika maagizo yangu, basi utaihukumu nyumba yangu, na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa haki ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Ukifuata mwongozo wangu na kuyazingatia maagizo niliyokupa, basi, utaisimamia nyumba yangu na nyua zake. Nami nitakuwezesha kuingia katika utumishi wangu kama hawa wanaosimama mbele yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kama utakwenda katika njia zangu na kuutumikia utumishi wangu, ndipo, wewe utakapoitunza Nyumba yangu na kuzilinda nyua zangu, kisha nitakupatia njia ya kufika kwangu katikati yao hawa wanaosimama hapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi asema hivi, Kama ukienda katika njia zangu, na kama ukishika maagizo yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba yangu, nawe utazilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi anasema hivi: Ukifuata njia zangu na kushika maagizo niliyokupa, basi, utaisimamia nyumba yangu na viwanja vyake. Nami nitakuwezesha kuingia katika utumishi wangu kama hawa wanaosimama mbele yangu.