Zechariah 3:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa sikiliza kwa makini, ewe Yoshua, kuhani mkuu; sikilizeni pia enyi makuhani wenzake mlio pamoja naye, nyinyi mlio ishara ya wakati mzuri ujao: Nitamleta mtumishi wangu aitwaye Tawi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninaenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako waketio mbele yako; maana hao ni watu walio ishara; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa sikiliza kwa makini, ewe Yoshua, kuhani mkuu; sikilizeni pia enyi makuhani wenzake mlio pamoja naye, nyinyi mlio ishara ya wakati mzuri ujao: Nitamleta mtumishi wangu aitwaye Tawi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Sikiliza, Ee Yoshua Kuhani Mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako wanaoketi mbele yako; maana hao ni watu walio ishara ya mambo yajayo; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa sikiliza kwa makini, ewe Yoshua, kuhani mkuu; sikilizeni pia enyi makuhani wenzake mlio pamoja naye, nyinyi mlio ishara ya wakati mzuri ujao: Nitamleta mtumishi wangu aitwaye Tawi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa sikia, wewe mtambikaji mkuu Yosua pamoja na wenzako wanaokaa mbele yako, kwani ndio watu wa kutazamiwa: Mtaniona, nikimleta mtumishi wangu Chipukizi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako waketio mbele yako; maana hao ni watu walio ishara; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa sikiliza kwa uangalifu, ewe Yoshua, Kuhani Mukubwa; musikilize vilevile enyi makuhani wenzake munaokuwa pamoja naye, ninyi munaokuwa kitambulisho cha wakati muzuri unaokuja: Nitamuleta mutumishi wangu anayeitwa Tawi.