Zechariah 3:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kumbukeni kuwa nimeweka mbele ya Yoshua jiwe moja lenye nyuso saba. Nami nitachora maandishi juu yake, na kwa siku moja tu, nitaiondoa dhambi ya nchi hii. Naam, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya Yoshua; katika jiwe moja yako macho saba; tazama, nitachora machoro yake, asema Bwana wa majeshi, nami nitauondoa uovu wa nchi ile katika siku moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kumbukeni kuwa nimeweka mbele ya Yoshua jiwe moja lenye nyuso saba. Nami nitachora maandishi juu yake, na kwa siku moja tu, nitaiondoa dhambi ya nchi hii. Naam, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya Yoshua; katika jiwe moja ziko nyuso saba; tazama, nitachonga maandishi yake, asema BWANA wa majeshi, nami nitauondoa uovu wa nchi hii katika siku moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kumbukeni kuwa nimeweka mbele ya Yoshua jiwe moja lenye nyuso saba. Nami nitachora maandishi juu yake, na kwa siku moja tu, nitaiondoa dhambi ya nchi hii. Naam, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani tazameni: Jiwe hili, nililoliweka mbele yake Yosua, macho saba yanalielekea jiwe hili moja; tena tazameni: Mimi ninachora humo machoro yanayolipasa, kisha nitaziondoa manza za nchi hii katika siku moja; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya Yoshua; katika jiwe moja yako macho saba; tazama, nitachora machoro yake, asema BWANA wa majeshi, nami nitauondoa uovu wa nchi ile katika siku moja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukumbuke kwamba nimeweka mbele ya Yoshua jiwe moja lenye nyuso saba. Nami nitachora maandiko juu yake, na kwa siku moja tu, nitaiondoa zambi ya inchi hii. Kweli, ni mimi Yawe wa majeshi ninayesema hivyo.