Zechariah 4:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo malaika akaniambia, “Hizo taa saba ni macho saba ya Mwenyezi-Mungu yaonayo kila mahali duniani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ni nani atakayeidharau siku ya mambo madogo? Macho saba ya Mwenyezi Mungu, yanayozunguka dunia yote, yatashangilia yatakapoona jiwe la juu kabisa likiwa mkononi mwa Zerubabeli!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayadharau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi.” Huyo malaika akaniambia, “Hizo taa saba ni macho saba ya Mwenyezi-Mungu yaonayo kila mahali duniani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli. “(Hizi saba ni macho ya BWANA ambayo huzunguka duniani kote.)”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli. “(Hizi saba ni macho ya bwana ambayo huzunguka duniani kote.)”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana yeyote aliyeidharau siku ya mambo madogo watafurahi, naye ataiona timazi ikiwa katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi taa saba ndizo macho ya BWANA; yanaona huku na huko duniani kote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo malaika akaniambia, “Hizo taa saba ni macho saba ya Mwenyezi-Mungu yaonayo kila mahali duniani.” Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayadharau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani walioibeua siku ya mambo madogo ndio watakaofurahi wakiiona timazi mkononi mwa Zerubabeli; hizi taa saba ndio macho ya Bwana, ndiyo yanayotembea katika nchi hii nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya BWANA; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayazarau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi. Sasa, juu ya hizo taa saba, yule malaika akaniambia: Ni macho saba ya Yawe yanayoona kila nafasi katika dunia.