Zechariah 4:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo akaniambia, “Matawi haya ndio wale watu wawili waliowekwa wakfu kwa mafuta wamtumikie Bwana wa ulimwengu wote.” Ahadi ya Mungu kwa Zerubabeli Naye akaniambia pia niseme neno hili la Mwenyezi-Mungu kumhusu Zerubabeli: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Huwezi kushinda kwa nguvu au kwa uwezo wako mwenyewe, bali kwa msaada wa roho yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.” Tena, akaongeza kusema: “Je, mlima huu ni kizuizi? La! Wewe Zerubabeli utausawazisha. Wewe utaanzisha ujenzi mpya wa hekalu, na wakati utakapoliweka jiwe la mwisho, watu watashangilia wakisema, ‘Ni zuri! Naam, ni zuri!’” Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia: “Zerubabeli ameuweka msingi wa hekalu naye pia atalikamilisha. Hayo yatakapotukia, watu wangu watajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndimi niliyekutuma kwao. Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayadharau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo akaniambia, “Matawi haya ndio wale watu wawili waliowekwa wakfu kwa mafuta wamtumikie Bwana wa ulimwengu wote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili watiwa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo akaniambia, “Matawi haya ndio wale watu wawili waliowekwa wakfu kwa mafuta wamtumikie Bwana wa ulimwengu wote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia: Hivi ndio wana wawili waliopakwa mafuta wanaosimama kwake Bwana wa nchi hii yote nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akaniambia: Hawa ndio wale watu wawili ambao Bwana wa ulimwengu wote aliwachagua kwa kuwapakaa mafuta kusudi wamutumikie.