Zechariah 4:9 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amenituma mimi kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Zerubabeli ameuweka msingi wa hekalu naye pia atalikamilisha. Hayo yatakapotukia, watu wangu watajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndimi niliyekutuma kwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa BWANA Mwenye Nguvu Zote amenituma mimi kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma mimi kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Zerubabeli ameuweka msingi wa hekalu naye pia atalikamilisha. Hayo yatakapotukia, watu wangu watajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndimi niliyekutuma kwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mikono yake Zerubabeli imeweka msingi wa Nyumba hii, nayo mikono yake ndiyo itakayoimaliza. Ndipo, utakapojua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma kwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zerubabeli ameuweka musingi wa hekalu naye vilevile atalikamilisha. Hayo yatakapotukia, watu wangu watajua kwamba mimi Yawe wa majeshi ndimi niliyekutuma kwao.