Zechariah 6:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye ndiye atakayelijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu Atapewa heshima ya kifalme na kuketi kwenye kiti chake cha enzi kuwatawala watu wake. Karibu na kiti cha enzi cha mtawala huyo, atakaa kuhani mkuu, nao wawili watafanya kazi pamoja kwa amani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni yeye atakayejenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki kwenye kiti cha enzi. Atakuwa kuhani kwenye kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa na amani kati ya hao wawili.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye ndiye atakayelijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu. Atapewa heshima ya kifalme na kuketi kwenye kiti chake cha enzi kuwatawala watu wake. Karibu na kiti cha enzi cha mtawala huyo, atakaa kuhani mkuu, nao wawili watafanya kazi pamoja kwa amani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni yeye atakayejenga Hekalu la BWANA, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni yeye atakayejenga Hekalu la bwana, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atakuwa na heshima ya kifalme; na ataketi na kutawala; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na maelewano yenye amani yatakuwa kati ya hao wawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye ndiye atakayelijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu Atapewa heshima ya kifalme na kuketi kwenye kiti chake cha enzi kuwatawala watu wake. Karibu na kiti cha enzi cha mtawala huyo, atakaa kuhani mkuu, nao wawili watafanya kazi pamoja kwa amani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli yeye ndiye atakayelijenga Jumba la Bwana na kujipatia utukufu; atakaa katika kiti chake cha kifalme na kutawala, tena atakuwa mtambikaji katika kiti chake cha kifalme, nalo shauri, hao wawili watakalolipiga, litakuwa la mapatano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye ndiye atakayelijenga hekalu la Yawe. Atapewa heshima ya kifalme na kuikaa kwenye kiti chake cha kifalme kuwatawala watu wake. Kuhani Mukubwa ataikaa karibu na kiti cha kifalme cha mutawala yule, nao wawili watafanya kazi pamoja kwa amani.