Zechariah 6:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu wanaokaa nchi za mbali watakuja kusaidia kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.” Nanyi mtajua kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, nanyi mtajua kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa bidii.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la Bwana, nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya Bwana, Mungu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu wanaokaa nchi za mbali watakuja kusaidia kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.” Nanyi mtajua kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kwamba BWANA Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii BWANA Mungu wenu kwa bidii.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la bwana, nanyi mtajua ya kwamba bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa bidii.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walio mbali watakuja na kusaidia kujenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu wanaokaa nchi za mbali watakuja kusaidia kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.” Nanyi mtajua kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao walioko mbali watakuja kusaidia kulijenga Jumba la Bwana. Ndipo, mtakapojua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma kwenu. Haya yatatimia, mkiisikia sauti ya Bwana Mungu wenu na kuitii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wanaokaa katika inchi za mbali watakuja kusaidia kwa kulijenga hekalu langu mimi Yawe. Nanyi mutajua kwamba Yawe wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mukiitii sauti ya Yawe, Mungu wenu.