Zechariah 8:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kabla ya wakati huo, watu hawakupata mshahara kwa kazi zao wala kwa kukodisha mnyama. Hamkuwa na usalama kwa sababu ya adui zenu, maana nilisababisha uhasama kati ya watu wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kabla ya wakati huo, hapakuwa na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kabla ya siku zile hapakuwa na ijara kwa mwanadamu, wala hapakuwa na ijara kwa mnyama; wala hapakuwa na amani kwake yeye aliyetoka, wala kwake yeye aliyeingia, kwa sababu ya adui; nami nalimwacha kila mtu kugombana na jirani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kabla ya wakati huo, watu hawakupata mshahara kwa kazi zao wala kwa kukodisha mnyama. Hamkuwa na usalama kwa sababu ya adui zenu, maana nilisababisha uhasama kati ya watu wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kabla ya siku zile hapakuwa na ijara kwa mwanadamu, wala hapakuwa na ijara kwa mnyama; wala hapakuwa na amani kwake yeye aliyetoka, wala kwake yeye aliyeingia, kwa sababu ya adui; nami nilimwacha kila mtu kugombana na jirani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kabla ya wakati huo, watu hawakupata mshahara kwa kazi zao wala kwa kukodisha mnyama. Hamkuwa na usalama kwa sababu ya adui zenu, maana nilisababisha uhasama kati ya watu wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kabla ya siku hizi hakikuwako kitu, watu walichokipata kwa kazi zao, wala hakikuwako, nyama walichokipata kwa kazi zao, tena kwa ajili ya kupingana hawakupata kutengemana wala aliyetoka wala aliyeingia, maana naliwachochea watu wote, wagombane kila mtu na mwenziwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kabla ya siku zile hapakuwa na ijara kwa mwanadamu, wala hapakuwa na ijara kwa mnyama; wala hapakuwa na amani kwake yeye aliyetoka, wala kwake yeye aliyeingia, kwa sababu ya adui; nami nalimwacha kila mtu kugombana na jirani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbele ya wakati huo, watu hawakupata mushahara kwa kazi zao wala mali kwa ajili ya kutumikisha nyama. Hamukuwa na usalama kwa sababu ya waadui zenu, maana nilisababisha uadui kati ya watu wote.