Zechariah 9:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atatokomeza magari ya vita nchini Efraimu, na farasi wa vita kutoka mjini Yerusalemu; pinde za vita zitavunjiliwa mbali. Naye ataleta amani miongoni mwa mataifa; utawala wake utaenea toka bahari hata bahari, toka mto Eufrate hata miisho ya dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, nao upinde wa vita utavunjwa. Atatangaza amani kwa mataifa. Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, na kutoka Mto hadi mwisho wa dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atatokomeza magari ya vita nchini Efraimu, na farasi wa vita kutoka mjini Yerusalemu; pinde za vita zitavunjiliwa mbali. Naye ataleta amani miongoni mwa mataifa; utawala wake utaenea toka bahari hata bahari, toka mto Eufrate hata miisho ya dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, nao upinde wa vita utavunjwa. Atatangaza amani kwa mataifa. Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, na kutoka Mto Eufrati hadi mwisho wa dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, nao upinde wa vita utavunjwa. Atatangaza amani kwa mataifa. Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiria mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atatokomeza magari ya vita nchini Efraimu, na farasi wa vita kutoka mjini Yerusalemu; pinde za vita zitavunjiliwa mbali. Naye ataleta amani miongoni mwa mataifa; utawala wake utaenea toka bahari hata bahari, toka mto Eufrate hata miisho ya dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nitakapoyatowesha magari kule Efuraimu, nao farasi mle Yerusalemu, nazo pindi za vita zitatoweshwa, nao wamizimu atawafundisha kutengemana; ufalme wake utaanzia baharini, uifikie bahari ya pili, tena uanzie penye jito kubwa, uyafikie mapeo ya nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ataondoa kabisa magari ya vita katika inchi ya Efuraimu, na farasi wa vita kutoka katika Yerusalema; pinde za vita zitatupwa mbali. Naye ataleta amani kati ya mataifa; utawala wake utaenea toka bahari mpaka bahari, toka muto Furati hata miisho ya dunia.