Zephaniah 1:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo nitaupekua mji wa Yerusalemu kwa taa, nitawaadhibu wanaoishi wametulia kama machicha ya divai, wote ambao husema mioyoni mwao: ‘Mwenyezi-Mungu hatafanya kitu: Chema au kibaya.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo nitaupekua mji wa Yerusalemu kwa taa, na kuwaadhibu wale ambao wanakaa katika hali ya kuridhika, ambao ni kama divai iliyobaki kwenye machicha, ambao hudhani, ‘Mwenyezi Mungu hatafanya lolote, jema au baya.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo nitaupekua mji wa Yerusalemu kwa taa, nitawaadhibu wanaoishi wametulia kama machicha ya divai, wote ambao husema mioyoni mwao: ‘Mwenyezi-Mungu hatafanya kitu: chema au kibaya.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo nitasaka katika mji wa Yerusalemu kwa taa na kuwaadhibu wale ambao wanakaa katika hali ya kuridhika, ambao ni kama divai iliyobaki kwenye machicha, ambao hudhani, ‘BWANA hatafanya lo lote, jema au baya.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo nitasaka mji wa Yerusalemu kwa taa, na kuwaadhibu wale ambao wanakaa katika hali ya kuridhika, ambao ni kama divai iliyobaki kwenye machicha, ambao hudhani, ‘ bwana hatafanya lolote, jema au baya.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya masira yao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo nitaupekua mji wa Yerusalemu kwa taa, nitawaadhibu wanaoishi wametulia kama machicha ya divai, wote ambao husema mioyoni mwao: ‘Mwenyezi-Mungu hatafanya kitu: Chema au kibaya.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hizo itakuwa, nitakapochunguzia Yerusalemu kwa mienge ya moto, niwavumbue wajikaliao tu penye shimbi za mvinyo zao na kusema mioyoni mwao: Bwana hafanyi wala mema wala mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo nitauchunguza Yerusalema kwa taa, nitawaazibu wanaoishi wakitulia kama machicha ya divai, wote ambao wanasema kati yao: Yawe hatafanya kitu: chema au kibaya.