Zephaniah 1:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Kwa moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa. Kwa ukamilifu na kwa namna ya kutisha atawafanya wakazi wote duniani watoweke.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Fedha yao wala dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Katika moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa, kwa maana ghafula ataleta mwisho wa wote wanaoishi duniani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Kwa moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa. Kwa ukamilifu na kwa namna ya kutisha atawafanya wakazi wote duniani watoweke.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Fedha yao wala dhahabu yao haitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya BWANA. Katika moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa, kwa maana ataleta mwisho wa wote wanaoishi katika dunia ghafula.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Fedha yao wala dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya bwana. Katika moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa, kwa maana ataleta mwisho wa wote wanaoishi katika dunia ghafula.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Kwa moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa. Kwa ukamilifu na kwa namna ya kutisha atawafanya wakazi wote duniani watoweke.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata fedha zao na dhahabu zao hazitaweza kuwaponya siku hiyo ya machafuko ya Bwana; katika moto wa wivu wake nchi hii yote nzima itateketea, kwani wote wakaao katika nchi hii atawaishiliza wote pia, wakiguiwa na kituko kwa mara moja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Feza yao wala zahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya kasirani ya Yawe. Kwa moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa. Kwa ukamilifu na kwa namna ya kuogopesha atawafanya wakaaji wote katika dunia watoweke.