Zephaniah 1:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaunyosha mkono wangu dhidi ya nchi ya Yuda, kadhalika na wakazi wote wa mji wa Yerusalemu. Nitaangamiza mabaki yote ya Baali kutoka nchi hii, na hakuna atakayetambua jina lao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nitaiadhibu Yuda na wote wanaoishi Yerusalemu. Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali kila mabaki ya Baali, majina ya wapagani na makuhani waabuduo sanamu:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaunyosha mkono wangu dhidi ya nchi ya Yuda, kadhalika na wakazi wote wa mji wa Yerusalemu. Nitaangamiza mabaki yote ya Baali kutoka nchi hii, na hakuna atakayetambua jina lao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nitaiadhibu Yuda na wote wakaao Yerusalemu. Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali kila mabaki ya Baali, majina ya wapagani na makuhani waabuduo sanamu:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nitaiadhibu Yuda na wote wakaao Yerusalemu. Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali kila mabaki ya Baali, majina ya wapagani na makuhani waabuduo sanamu:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaunyosha mkono wangu dhidi ya nchi ya Yuda, kadhalika na wakazi wote wa mji wa Yerusalemu. Nitaangamiza mabaki yote ya Baali kutoka nchi hii, na hakuna atakayetambua jina lao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitaukunjua mkono wangu, uwakamate Wayuda nao wote wakaao Yerusalemu; masao yote ya Baali nitayatowesha mahali hapa, majina yao watangazaji pamoja nayo ya watambikaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitaunyoosha mukono wangu kwa kuazibu inchi ya Yuda, pamoja na wakaaji wote wa Yerusalema. Nitaangamiza mabaki yote ya mungu Bali kutoka inchi hii, na hakuna atakayetambua jina lao.