Zephaniah 2:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atakuwa wa kutisha dhidi yao; miungu yote ya dunia ataikondesha. Mataifa yote duniani yatamsujudia; kila taifa katika mahali pake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atakuwa wa kuhofisha kwao atakapoangamiza miungu yote ya nchi. Mataifa katika kila pwani yatamwabudu, kila moja katika nchi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atakuwa wa kutisha dhidi yao; miungu yote ya dunia ataikondesha. Mataifa yote duniani yatamsujudia; kila taifa katika mahali pake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atakuwa wa kutisha kwao wakati atakapoangamiza miungu yote ya nchi. Mataifa katika kila pwani yatamwabudu, kila moja katika nchi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atakuwa wa kuhofisha kwao atakapoangamiza miungu yote ya nchi. Mataifa katika kila pwani yatamwabudu, kila moja katika nchi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA atakuwa wa kutisha sana kwao; kwa maana atawaua kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atakuwa wa kutisha dhidi yao; miungu yote ya dunia ataikondesha. Mataifa yote duniani yatamsujudia; kila taifa katika mahali pake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ataogopwa kwao, kwani miungu yote ya hapa nchini ataitowesha, wamwangukie wote, kila mtu mahali pake, hata visiwa vyote vya wamizimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao watamwogopa sana Yawe; ataiangamiza miungu yote ya dunia. Mataifa yote katika dunia yatamwabudu; kila taifa katika pahali pake.