Zephaniah 2:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makundi ya mifugo yatalala humo, kadhalika kila mnyama wa porini. Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake, bundi watalia kwenye madirisha yake, kunguru watalia kwenye vizingiti, maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makundi ya kondoo na ng’ombe yatajilaza pale, viumbe vya kila aina. Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba wataishi juu ya nguzo zake. Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani, kifusi kitakuwa milangoni, boriti za mwerezi zitaachwa wazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makundi ya mifugo yatalala humo, kadhalika kila mnyama wa porini. Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake, bundi watalia kwenye madirisha yake, kunguru watalia kwenye vizingiti, maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makundi ya kondoo na ng'ombe yatajilaza pale, viumbe vya kila aina. Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba wataishi juu ya nguzo zake. Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani, kifusi kitakuwa milangoni, boriti za mierezi zitaachwa wazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makundi ya kondoo na ng’ombe yatajilaza pale, viumbe vya kila aina. Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba wataishi juu ya nguzo zake. Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani, kifusi kitakuwa milangoni, boriti za mierezi zitaachwa wazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; bundi na kunguru watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makundi ya mifugo yatalala humo, kadhalika kila mnyama wa porini. Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake, bundi watalia kwenye madirisha yake, kunguru watalia kwenye vizingiti, maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwake yatalala makundi mazima ya kila nyama wa nchi za mataifa, hata korwa na nungu watalala katika vichwa vya nguzo zake, sauti za bundi zitasikilika madirishani, penye vizingiti patajaa takataka, kwani mbao za miangati zitakuwa zimeondolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makundi ya nyama wa kufugwa watalala ndani yake, vilevile kila nyama wa pori. Tai, nyangenyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake, bundi watalia kwenye madirisha yake, vibombobombo watalia kwenye vizingiti, maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu.