Zephaniah 2:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nchi ya pwani itamilikiwa na mabaki ya ukoo wa Yuda. Watachunga mifugo yao huko. Nyumba za mji wa Ashkeloni zitakuwa mahali pao pa kulala. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wao atawakumbuka na kuwarudishia hali yao njema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, hapo watapata malisho. Wakati wa jioni watajilaza chini katika nyumba za Ashkeloni. Mwenyezi Mungu, Mungu wao, atawatunza, naye atawarudishia wafungwa wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana Bwana, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wafungwa wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nchi ya pwani itamilikiwa na mabaki ya ukoo wa Yuda. Watachunga mifugo yao huko. Nyumba za mji wa Ashkeloni zitakuwa mahali pao pa kulala. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wao atawakumbuka na kuwarudishia hali yao njema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, hapo watapata malisho. Wakati wa jioni watajilaza chini katika nyumba za Ashkeloni. BWANA Mungu wao atawatunza, naye atawarudishia wafungwa wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, hapo watapata malisho. Wakati wa jioni watajilaza chini katika nyumba za Ashkeloni. bwana Mwenyezi Mungu wao atawatunza, naye atawarudishia wafungwa wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watachunga makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajia na kuwarudisha wafungwa wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nchi ya pwani itamilikiwa na mabaki ya ukoo wa Yuda. Watachunga mifugo yao huko. Nyumba za mji wa Ashkeloni zitakuwa mahali pao pa kulala. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wao atawakumbuka na kuwarudishia hali yao njema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nchi hii itakuwa yao wakaosalia wa mlango wa Yuda; wao ndio watakaochunga huko, tena jioni watakwenda kulala katika nyumba za Askaloni; kwani Bwana Mungu wao atawakagua, ayafungue tena mafungo yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wafungwa wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inchi ya pembeni ya bahari itakuwa makao ya mabaki ya ukoo wa Yuda. Watachunga nyama wao kule. Nyumba za muji wa Askeloni zitakuwa pahali pao pa kulala. Maana mimi Yawe, Mungu wao nitawakumbuka na kuwarudishia hali yao njema.