Zephaniah 2:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, mimi Mungu wa Israeli, Moabu itakuwa kama Sodoma na Amoni itakuwa kama Gomora. Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara, watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakika, kama niishivyo,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, Waamoni kama Gomora: mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, nchi ya ukiwa milele. Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kama niishivyo, asema Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, mimi Mungu wa Israeli, Moabu itakuwa kama Sodoma na Amoni itakuwa kama Gomora. Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara, watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakika, kama niishivyo,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, Waamori kama Wagomora: mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, nchi ya ukiwa milele. Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakika, kama niishivyo,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, Waamoni kama Gomora: mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, nchi ya ukiwa milele. Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, mimi Mungu wa Israeli, Moabu itakuwa kama Sodoma na Amoni itakuwa kama Gomora. Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara, watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli: Kweli kwa hivyo, nilivyo Mwenye uzima, nchi ya Moabu itakuwa kama Sodomu nayo nchi ya wana wa Amoni kama Gomora, zitageuka kuwa kwenye viwawi, zitakuwa mashimo ya chumvi na mapori matupu kale na kale. Masao yao walio ukoo wangu watawanyang'anya mali zao, watakaosalia wa taifa langu watawachukua, wawe watumwa wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli– inchi ya Moabu itakuwa kama Sodoma na ya Amoni itakuwa kama Gomora. Inchi zake zitakuwa shamba la miiba na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka, watu wa taifa langu waliobaki watazirizi.