Zephaniah 3:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku hiyo, haitakulazimu kuona aibu, kutokana na matendo yako ya kuniasi, maana nitawaondoa miongoni mwako wale wanaojigamba na kujitukuza nawe hutakuwa na kiburi tena katika mlima wangu mtakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku hiyo hutaaibishwa kwa ajili ya makosa yote uliyonitendea, kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huu wale wote wanaoshangilia katika kiburi chao. Kamwe hutajivuna tena katika kilima changu kitakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku ile hutatahayarikia matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaotakabari na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku hiyo, haitakulazimu kuona aibu, kutokana na matendo yako ya kuniasi, maana nitawaondoa miongoni mwako wale wanaojigamba na kujitukuza nawe hutakuwa na kiburi tena katika mlima wangu mtakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku hiyo hutaaibishwa kwa ajili ya makosa yote ulionitendea, kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huu wale wote wanaoshangilia katika kiburi chao. Kamwe hutajivuna tena katika kilima changu kitakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku hiyo hutaaibishwa kwa ajili ya makosa yote ulionitendea, kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huu wale wote wanaoshangilia katika kiburi chao. Kamwe hutajivuna tena katika kilima changu kitakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku ile hutaaibishwa kwa matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaojigamba na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku hiyo, haitakulazimu kuona aibu, kutokana na matendo yako ya kuniasi, maana nitawaondoa miongoni mwako wale wanaojigamba na kujitukuza nawe hutakuwa na kiburi tena katika mlima wangu mtakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo hutapatwa na soni kwa ajili ya matendo yako yote, uliyonikosea, kwani hapo ndipo, nitakapowaondoa katikati yako walioyafurahia majivuno yako, usiendelee tena kujikuza mlimani penye Patakatifu pangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku ile hutatahayarikia matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaotakabari na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, hautapata haya kutokana na matendo yako ya kuniasi, maana nitawaondoa kati yako wale wanaojivuna na kujitukuza, nawe hautakuwa na kiburi tena kwenye mulima wangu mutakatifu.