Zephaniah 3:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu amekuondolea hukumu iliyokukabili, amewageuzia mbali adui zako. Mwenyezi-Mungu, mfalme wa Israeli yuko pamoja nawe hutaogopa tena maafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu amekuondolea adhabu yako, amewarudisha nyuma adui zako. Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Israeli, yu pamoja nawe; kamwe hutaogopa tena madhara yoyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana ameziondoa hukumu zako, Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana, yu katikati yako; Hutaogopa uovu tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu amekuondolea hukumu iliyokukabili, amewageuzia mbali adui zako. Mwenyezi-Mungu, mfalme wa Israeli yuko pamoja nawe hutaogopa tena maafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA amekuondolea adhabu yako, amewarudisha nyuma adui zako. BWANA, Mfalme wa Israeli, yu pamoja nawe; kamwe hutaogopa tena madhara yo yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana amekuondolea adhabu yako, amewarudisha nyuma adui zako. bwana, Mfalme wa Israeli, yu pamoja nawe; kamwe hutaogopa tena madhara yoyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA ameziondoa hukumu zako, Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa Israeli, naam, yeye BWANA, yuko katikati yako; Hutaogopa uovu tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu amekuondolea hukumu iliyokukabili, amewageuzia mbali adui zako. Mwenyezi-Mungu, mfalme wa Israeli yuko pamoja nawe hutaogopa tena maafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ameyatangua mashauri, uliyokatiwa, akamwondoa adui yako! Mfalme wa Isiraeli ni Bwana alioko katikati yako, hutaogopa mabaya tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA ameziondoa hukumu zako, Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa Israeli, naam, yeye BWANA, yu katikati yako; Hutaogopa uovu tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe amekuondolea hukumu iliyokuwa juu yako, amewafukuza waadui zako. Yawe, mufalme wa Israeli yuko pamoja nawe. Hautaogopa tena hasara.