Zephaniah 3:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, nitawaadhibu wote wanaokukandamiza. Nitawaokoa vilema na kuwakusanya waliotupwa, na kubadili aibu yao kuwa sifa na fahari duniani kote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo nitawaadhibu wote waliokudhulumu; nitaokoa vilema na kukusanya wale waliotawanywa. Nitawapa sifa na heshima katika kila nchi ambayo waliaibishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, nitawaadhibu wote wanaokukandamiza. Nitawaokoa vilema na kuwakusanya waliotupwa, na kubadili aibu yao kuwa sifa na fahari duniani kote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika wakati huo nitawashughulikia wote waliokudhulumu; nitaokoa kilema na kukusanya wale ambao wametawanywa. Nitawapa sifa na heshima katika kila nchi ambamo waliaibishwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo nitawashughulikia wote waliokudhulumu; nitaokoa vilema na kukusanya wale ambao wametawanywa. Nitawapa sifa na heshima katika kila nchi ambayo waliaibishwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya msifiwe na kujulikana, hao ambao aibu yao ilikuwa katika dunia yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, nitawaadhibu wote wanaokukandamiza. Nitawaokoa vilema na kuwakusanya waliotupwa, na kubadili aibu yao kuwa sifa na fahari duniani kote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaniona, siku hizo nikiwapatia mambo wote wanaokutesa, niwaokoe wachechemeao, niwakusanye nao waliofukuzwa, watukuzwe, nikiwapatia jina kuu katika hizo nchi zote, walikotiwa soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo, nitawaazibu wote wanaokugandamiza. Nitawaokoa vilema na kuwakusanya waliotupwa na kubadilisha haya yao kuwa sifa na utukufu katika dunia yote.