Zephaniah 3:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo nitawakusanya, na kuwafanya mjulikane na kusifiwa, miongoni mwa watu wote duniani nitakapowarudishia hali yenu njema nanyi muone kwa macho yenu wenyewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo nitawakusanya; wakati huo nitawaleta nyumbani. Nitawapa sifa na heshima miongoni mwa mataifa yote ya dunia wakati nitakapowarudishia mateka yenu mbele ya macho yenu hasa,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi kuwa sifa na jina, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo nitawakusanya, na kuwafanya mjulikane na kusifiwa, miongoni mwa watu wote duniani nitakapowarudishia hali yenu njema nanyi muone kwa macho yenu wenyewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo nitawakusanya; wakati huo nitawaleta nyumbani. Nitawapa sifa na heshima miongoni mwa mataifa yote ya dunia wakati nitakapowarudishia mateka yenu mbele ya macho yenu hasa,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo nitawakusanya; wakati huo nitawaleta nyumbani. Nitawapa sifa na heshima miongoni mwa mataifa yote ya dunia wakati nitakapowarudishia mateka yenu mbele ya macho yenu hasa,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi msifiwe na mjulikane, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo nitawakusanya, na kuwafanya mjulikane na kusifiwa, miongoni mwa watu wote duniani nitakapowarudishia hali yenu njema nanyi muone kwa macho yenu wenyewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hizo ndipo, nitakapowapeleka kwenu ni siku hizo, nitakapokwisha kuwakusanya, kwani nitawapatia ninyi jina kuu, mtukuzwe kwa makabila yote ya nchi hii, nitakapoyafungua mafungo yenu machoni pao. Bwana ndiye anayeyasema!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi kuwa sifa na jina, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo nitawakusanya, na kuwafanya mujulikane na kusifiwa kati ya watu wote katika dunia, na kuwarudishia hali yenu njema, nanyi mutaona kwa macho yenu wenyewe. –Ni Yawe anayesema hivyo.