bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Ezekiel 12
Ezekiel 12
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 13 →
1
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
2
“Mwanadamu, unaishi miongoni mwa watu waasi. Wana macho ya kuona, lakini hawaoni, na masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa kuwa ni watu waasi.
3
“Kwa hiyo, mwanadamu, funga mizigo yako kwa kwenda uhamishoni tena wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toka nje na uende mahali pengine kutoka hapo ulipo. Huenda wataelewa, ingawa wao ni nyumba ya uasi.
4
Wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toa nje mizigo yako iliyofungwa kwa ajili ya kwenda uhamishoni. Kisha wakati wa jioni, wakiwa wanakutazama toka nje kama wale wanaoenda uhamishoni.
5
Wakiwa wanakutazama, toboa ukuta utolee mizigo yako hapo.
6
Beba mizigo hiyo begani mwako wakikuangalia uichukue nje wakati wa giza la jioni. Funika uso wako ili usione nchi, kwa maana nimekufanya ishara kwa nyumba ya Israeli.”
7
Basi nikafanya kama nilivyoamriwa. Wakati wa mchana nilitoa vitu vyangu nje vilivyofungwa tayari kwa uhamishoni. Kisha wakati wa jioni nikatoboa ukuta kwa mikono yangu. Nikachukua mizigo yangu nje wakati wa giza la jioni, nikiwa nimeibeba mabegani mwangu huku wakinitazama.
8
Asubuhi neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
9
“Mwanadamu, je, nyumba ile ya uasi ya Israeli haikukuuliza, ‘Unafanya nini?’
10
“Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Unabii huu unamhusu mkuu aliye katika Yerusalemu na watu wote wa nyumba ya Israeli walio huko.’
11
Waambie, ‘Mimi ni ishara kwenu.’ “Kama vile nilivyotenda, basi litatendeka vivyo hivyo kwao. Wataenda uhamishoni kama mateka.
12
“Mkuu aliye miongoni mwao atabeba mizigo yake begani wakati wa giza la jioni na kuondoka, na tundu litatobolewa ukutani ili apite. Atafunika uso wake ili asiweze kuiona nchi.
13
Nitamtandazia wavu wangu, naye atanaswa kwenye mtego wangu; nitamleta hadi Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona, naye atafia huko.
14
Wote wanaomzunguka nitawatawanya pande zote: watumishi wake na majeshi yake yote; nami nitawafuatilia kwa upanga.
15
“Wao watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapowatawanya miongoni mwa mataifa, na kuwatapanya katika nchi zote.
16
Lakini nitawaokoa wachache wao, wasiuawe kwa upanga, njaa na tauni, ili katika mataifa watakakoenda waweze kukiri matendo yao yote ya kuchukiza. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.”
17
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
18
“Mwanadamu, tetemeka unapokula chakula chako, tetemeka kwa hofu unapokunywa maji yako.
19
Waambie watu wa nchi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kuhusu wakaaji wa Yerusalemu na katika nchi ya Israeli: Watakula chakula chao kwa wasiwasi na kunywa maji yao kwa kufadhaika, kwa kuwa nchi yao itanyang’anywa kila kitu chake kwa sababu ya udhalimu wa wote wanaoishi humo.
20
Miji inayokaliwa na watu itaharibiwa na nchi itakuwa ukiwa. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
21
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
22
“Mwanadamu, ni ipi hii mithali mlio nayo katika nchi ya Israeli: ‘Siku zinapita na hakuna maono yoyote yanayotimia’?
23
Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia ambapo kila ono litatimizwa.
24
Kwa maana hapatakuwa tena na maono ya uongo wala ubashiri wa kujipendekeza miongoni mwa watu wa Israeli.
25
Lakini Mimi Mwenyezi Mungu nitasema neno nitakalo, nalo litatimizwa bila kuchelewa. Kwa kuwa katika siku zako, ewe nyumba ya uasi, nitatimiza kila nisemalo, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ”
26
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
27
“Mwanadamu, nyumba ya Israeli inasema, ‘Maono yale anayoyaona ni kwa ajili ya miaka mingi ijayo, naye hutabiri kuhusu siku zijazo zilizo mbali.’
28
“Kwa hiyo, waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakuna maneno yangu yatakayocheleweshwa tena zaidi, lolote nisemalo litatimizwa, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ”
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48