bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Ezekiel 13
Ezekiel 13
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 14 →
1
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
2
“Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno la Mwenyezi Mungu!
3
Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote!
4
Manabii wako, ee Israeli, ni kama mbweha katikati ya magofu.
5
Hamjakwea kwenda kuziba mahali palipobomoka katika ukuta ili kuukarabati kwa ajili ya nyumba ya Israeli, ili isimame imara kwenye vita katika siku ya Mwenyezi Mungu.
6
Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “Mwenyezi Mungu amesema”, wakati Mwenyezi Mungu hakuwatuma; bado wakitarajia maneno yao kutimizwa.
7
Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu, hapo msemapo, “Mwenyezi Mungu asema”, wakati Mimi sijasema?
8
“ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa sababu ya maneno yenu ya uongo na maono yenu ya udanganyifu, Mimi niko kinyume nanyi, asema Bwana Mungu Mwenyezi.
9
Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuorodheshwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli, wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi.
10
“ ‘Kwa sababu wanapotosha watu wangu, wakisema, “Amani”, wakati hakuna amani; pia kwa sababu, wakati ukuta dhaifu unapojengwa, wanaufunika kwa kupaka chokaa,
11
kwa hiyo waambie hao wanaoupaka chokaa isiyokorogwa vyema kwamba ukuta huo utaanguka. Mvua kubwa ya mafuriko itanyesha, nami nitaleta mvua ya mawe inyeshe kwa nguvu, nao upepo wa dhoruba utavuma juu yake.
12
Ukuta utakapoanguka, je, watu hawatawauliza, “Iko wapi chokaa mliyopaka ukuta?”
13
“ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika ghadhabu yangu nitauachia upepo wa dhoruba, na katika hasira yangu, mvua ya mawe na ya mafuriko itanyesha, ikiwa na ghadhabu ya kuangamiza.
14
Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
15
Hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu dhidi ya huo ukuta na dhidi yao walioupaka chokaa. Nitawaambia ninyi, “Ukuta umebomoka na vivyo hivyo wale walioupaka chokaa,
16
wale manabii wa Israeli walioitabiria Yerusalemu na kuona maono ya amani kwa ajili yake wakati hakukuwa na amani, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” ’
17
“Sasa, mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya binti za watu wako wanaotabiri mambo kutoka mawazo yao wenyewe. Tabiri dhidi yao
18
na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu?
19
Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwanenea uongo watu wangu, ambao husikiliza uongo, mmewaua watu ambao hawakustahili kufa, na kuwaacha hai wale ambao walistahili kufa.
20
“ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi mnazotumia kuwatega watu kama ndege, nami nitazirarua mikononi mwenu; nitawaweka huru watu mliowatega kama ndege.
21
Nitazirarua shela zenu na kuwaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu, nao hawatakuwa tena mawindo ya nguvu zenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
22
Kwa sababu mliwavunja moyo wenye haki kwa uongo wenu, wakati mimi sikuwaletea huzuni na kwa kuwa mliwatia moyo waovu ili wasiziache njia zao mbaya na hivyo kuokoa maisha yao,
23
kwa hiyo hamtaona tena maono ya uongo wala kufanya ubashiri. Nitawaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu. Nanyi ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48